WASHABIKI 11,056 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Coastal Union na Yanga lililochezwa juzi (Machi 31 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Viingilio katika pambano hilo vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP, sh. 6,000 jukwaa kuu na sh. 4,000 mzunguko. Mapato yaliyopatikana kwenye pambano hilo ni sh. 61,494,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 14,664,927.80 uwanja sh. 4,630,335.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (DRFA) sh. 2,515,494.37.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 4,630,335.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,315,167.97 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 463,033.59.
Nayo mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 29,716,000 kutokana na watazamaji 8,167 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo.
Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 4,532,949.15, kila timu ilipata sh. 5,031,085.25, Uwanja sh. 1,486,465.08, TFF sh. 1,486,465.08, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,084,600.03, FDF sh. 743,232.54 na BMT sh. 148,646.51.
Wakati huo huo; pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Ruvu Stars lililochezwa jana (Aprili Mosi mwaka huu) Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam limeingiza sh. 1,585,000.
Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 1,000 mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu ni 1,569.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 283,656, uwanja sh. 57,942, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 117,306.08, TFF sh. 57,942, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 28,971 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 5,794.02.