KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict 16, amewasili nchini Mexico huku akilakiwa na mamia ya waumini waliojipanga kwa kiasi cha umbali wa kilometa 20 katika njia aliyopitia katika Mji Mkuu wa nchi hiyo.
Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo za kumkaribisha papa Benedict huku wakisema, Benedict, kaka, sasa wewe ni Mmexico. Wengi wanafikiri makaribisho hayo mazuri, yakisindikizwa na muziki wa asili, wa Mariachis, usingepaswa kumlaki kiongozi huyo wa kidini kwa kuwa unaonekana kuwa nje ya maadili ya kidini na wa kisomi tu.
Lakini nchi hiyo yenye idadi kubwa ya waumuni wa kanisa Katoliki duniani, inayozungumza lugha ya Kihispoaniola, imemuonyesha papa Benedict mapenzi waliyonayo kwa mrithi wa kiti alichokalia pope John Paul wa 11, ambaye alionekana kuwa papa wa Mexico , wakati wa uhai wake baada ya kufanya ziara mara tano nchini humo.
Hii ni nchi yenye kujisikia fahari kwa ukarimu, na hakuna mtu ambaye anahisi kuwa mgeni katika nchi yenu, amesema papa wakati alipowasili huku akishangiliwa kwa nguvu.
Baada ya ndege yake kutua, mitaa ya Leon ambako pope atakaa, ilikuwa katika hali ya sherehe kubwa, ambapo majengo yote yaliripuka kwa kumwagiwa konfeti za rangi ya njano wakati akipita katika gari yake ambayo haiwezi kuathirika kwa bomu katika njia hiyo yenye urefu wa kilometa 32 kutoka uwanja wa ndege.
Amekuja kuwabadilisha Wamexicani wote, amesema Maria del Rosario Tamayo Villanueva, ambaye alitaka kumuona papa licha ya kuwa na ulemavu wa miguu yake yote tangu akiwa mtoto. Ilikuwa ni muhimu kuja kumuona. Ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Hapo mapema katika safari yake ya saa 14 kutoka mjini Rome, Benedict amewataka Wamexicani kupambana na hali ya kuabudu fedha, hali ambayo inasababisha ghasia zinazohusishwa na madawa ya kulevywa na kuitaka Cuba, ambako anaelekea huko siku ya Jumatatu, kuachana na nadharia za Kimaxi, ambazo zimepitwa na wakati.
Amezungumzia hapo kabla upinzani wake dhidi ya biashara ya madawa ya kulevywa, nadharia za kimaxi pamoja na udikteta katika eneo la Latin America, ikiwa ni pamoja na katika ziara yake ya mwaka 2007 nchini Brazil, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika eneo hilo.
Siku ya Ijumaa Rais wa Mexico Felipe Calderon na mkewe Margareta Zavala walimlaki papa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Guanajuto mjini Silao na kufuatana naye katika zulia jekundu huku kengele za kanisani zikilia.
Benedict aliteremka katika ngazi bila ya kutumia fimbo ambayo amekuwa akiitumia wakati alipoelekea katika ndege mjini Rome, ikiwa ni mara ya kwanza kutembea na fimbo hiyo hadharani.
-DW