Dunia yalaani mapinduzi Mali

Rais Amadou Toumani Toure wa Mali aliyepinduliwa

MATAIFA mbalimbali duniani yamelalamikia kitendo cha wanajeshi wa Mali kufanya uamuzi wa kuipindua Serikali ya Rais Amadou Toumani Toure.

Taarikutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limetaka utawala wa kikatiba kurejeshwa nchini humo mara moja, huku Benki ya Dunia pamoja na Benki ya Maendeleo barani Afrika wakisema wanasitisha baadhi ya shughuli nchini humo.

Msemaji wa wanajeshi waasi nchini Mali amesema jeshi litarejesha demokrasia nchini humo na kuwa umoja utarejea hivi karibuni.

Kufikia sasa haijulikani alipo Rais Amadou Toumani Toure, lakini taarifa ya televisheni ya taifa ilisema kuwa rais huyo yuko katika hali nzuri ya kiafya.
-BBC