Lowassa azungumza na walimu Sekondari ya Engutoto, Monduli

Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akizungumza kwa kusisitiza wakati wa mkutano wake na walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto, wilayani Monduli kuhusiana na hali ya elimu katika shule hiyo kutoridhisha baada ya wanafunzi wengi kufeli kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne. Mkutano huo umefanyika leo shuleni hapo, ambapo walimu wa shule hiyo walitoa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Lowassa amewaasa walimu kufanya kazi kwa juhudi ili kuwaandaa vijana wa taifa la baadae. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Joseph Lukumay.

Ofisa Elimu Wilaya ya Monduli, Shaaban Mngunye (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa (wa pili kulia) wakati wa mkutano na walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto, wilayani Monduli. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Ally Muyago na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Joseph Lukumay.

Walimu wa Shule ya Engutoto iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha, wakizungumzia changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kazi yao ambapo wengi wamedai kuwa inachangia kwa kiasi fulani kudhorota kwa elimu katika shule hiyo.