Na Mwandishi Wetu
MWANAMUZIKI maarufu wa bendi kongwe ya Msondo ngoma, Muhidin Gurumo aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo la damu anaendelea vizuri.
Akizungumzia afya hiyo jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’ alisema; Gurumo anaendelea vizuri na wakati wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini. Alisema madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kujua kila kitu kinachomsumbua katika mwili wake.
“Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti
na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivi
karibuni,” alisema Super D.
Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo kumuombea duwa mwanamziki huyo ili apone upesi pia aliongeza kwa kusema maonesho yao ya wikii hii ni kama ifuatavyo Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani, Ijumaa watapiga katika viwanja vya Lidaz Clab jumamosi watakuwa katika viwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wiki endi katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni alisema Super D.