Alietengeneza filamu ya Joseph Kony arukwa na akili

Jason Russell

MKURUGENZI wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake inayomshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye mtandao wa internet, inanaiwa amepata ugonjwa wa akili.

Shirika lililofanya filamu hiyo, liitwalo “Invisible Children”, limesema kuwa Russell amelazwa hospitali kutokana na machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa.

Shirika la “Invisible Children”, lilisema zogo lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za wanachama wote; na hasa Russell.

Ripoti zinasema kuwa Jason Russell amekutikana akiwa amevaa vibaya (hakujistiri) huku akipiga kelele hovyo barabarani mjini San Diego, California.

Filamu hiyo ya nusu saa, iliyotoa wito kuwa Joseph Kony akamatwe, ilizagaa kwenye mitandao, na kuwasikitisha wengi, lakini baadhi ya watu wanaona filamu haikueleza vita vya Uganda vilivyo.
-BBC