KIMD ilipoanza ujenzi wa daraja la Iteba Dar es Salaam

Meneja Miradi wa KIMD Constructor, Onesmo Nathan akimwelezea jambo kuhusiana na ujenzi wa daraja la watembea kwa Mguu la ITEBA linalounganisha Sinza na Manzese jijini Dar es Salaam linalojengwa na kampuni hiyo KIMD kutoka Mjini Kibaha mkoani Pwani. KIMD ni moja ya kampuni chache za Ujenzi zinazomilikiwa na wazawa kwa 100% na imekuwa ikifanya kazi nyingi za ujenzi wa barabara, mashule, na vituo vya afya katika maeneo mengi hasa Mkoani Pwani.

Watoto washule wakipita katika daraja la muda lililowekwa na vijana wa Manzese katika Mto Iteba unaotenganisha Sinza na Manzese jijini Dar es Salaam. Pem,beni ni ujenzi wa daraja la kudumu ulioanza kufanyika hivi karibuni chini ya Kampuni ya Ujenzi ya KIMD kutoka Kibaha mkoani Pwani.