MUVI yatoa mafunzo kwa maofisa kilimo wilayani Mbinga

Mkaguzi wa Mbegu, Donasian Shayo akitoa mafunzo kwa maofisa ugani wilayani Mbinga.

MUUNGANISHO wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) Mkoa wa Ruvuma hivi karibuni umetoa mafunzo kwa maofisa ugani (mabwana/mabibi shamba) wa Wilaya ya Mbinga.

Hiyo ni moja ya jitihada za mradi huo kuhakikisha wakulima wa alizeti na mhogo katika mkoa huo wanapata elimu stahiki kuhusu ulimaji na utunzaji wa mazao hayo ambayo yana soko la uhakika mkoani Ruvuma.

Akitoa mafunzo hayo Mkaguzi wa Ubora wa Mbegu kutoka Taasisi ya Ukaguzi na Ubora wa Mbegu Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ‘Organisation Seeds Certification Institution’ (TOSCI), Donasian Shayo amewataka maofisa hao kuwa karibu na wakulima ikiwa ni pamoja na kuwasaidia.

Hata hivyo mkufunzi huyo alisema ili waweze kupata mavuno mengi na bora,maafisa hao hawana budi kuwa makini na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kugundua kwa haraka mbegu ambazo zinaweza kuwasaidia wakulima.

Naye Bi. Magreth Mkuchu amewambia wawakilishi wa wakulima hao ambao wapo katika mradi wa MUVI na wale wa waliyo teuliwa kuwa na mashamba ya mfano ya mbegu bora kusambaza elimu hiyo kwa wengine nakufuatisha mpango kazi.

Maofisa hao walisema kuwa endapo wangekuwa wakipata mafunzo hayo mara kwa mara kama walivyopata kutoka MUVI watakuwa wakiwakilisha mbinu mpya kwa wakulima ikizingatiwa mambo mengi yamebadilika na sasa kilimo ni biashara.

Semina hiyo iliandaliwa hivi karibuni na mradi wa Muvi na wakufunzi wa mafunzo hayo wakitokea Kituo cha utafiti wa kilimo Uyole Mbeya na Taasisi ya udhibiti wa ubora wa mbegu (TISCI )ya Njombe.

Miongoni mwa maofisa waliyo shiriki katika semina hiyo ni baadhi ya kata zilizopo katika mradi huo na za jirani na vijiji vilivyomo ambazo ni Mkako, Kigongsera, Mtama, Kilosa, Mbababay, Maguu, Mbinga mjini.

Haya yote yanafanyika ili kuweza kueneza dhana ya mnyororo wa thamani hususani katika zao la mhogo na alizeti ambalo ndiyo mazao yanayo shughulikiwa na Mradi wa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) Hata hivyo mafunzo kama hayo yamefanyika wilaya za Namtumbo na Songea Vijijini