*Ni mshindi wa mwenzi promosheni ya Nani Mkali
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na wigo mpana wa mawasiliano, leo imemzawadia mshindi wa kwanza wa mwenzi wa promosheni ya “Nani Mkali”, Abdi Ibrahim Mohamed mkazi wa Muheza Tanga sh. milioni 30.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano Ofisa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Dangio Kaniki amesema kampuni hiyo inamzawadia Bwana Mkali Ibrahim Mohamed kitita cha milioni 30 baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo.
“Kama mnavyofahamu tumekuwa tukitangaza washindi wa siku na wa wiki, Airtel bado inawapa nafasi nyingine Watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya sh. milioni 200, kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya ‘Nani Mkali’,” alisema.
Aidha alisema Airtel itaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wake inchi nzima na kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, ili kujiunga na “Nani Mkali”, mteja anatakiwa kuandika neno “Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa.
“Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10. Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi. aliongeza Kaniki. Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo, Abdi Ibrahim Mohamed alisema” nachukua fulsa hii kuwashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuanzisha promosheni hii na najisikia furaha kuibuka Mkali wa Airtel na kujishindia pesa taslimu shilling milion 30 leo hii.”
Napenda kutoa wito kwa wateja wa Airtel kushiriki na wale ambao hawajajiunga kushiriki na kuibuka washindi kama nilivyojishindia leo, kila mmoja ananafasi ya kushiriki na Kushinda kama mimi nimeshinda toka Tanga wilayani muheza hii inaonyesha wazi kuwa nafasi ipo kubwa kwa kila mtanzania Kushinda awe wa mjini au vijijini.