Mamia wauawa Sudan Kusini kwa kisasi

Wapiganaji Sudan Kusini

WATU takriban 100 wameuawa Sudan Kusini katika mfululizo wa mauaji ya kikabila hivi karibuni na wizi wa mifugo, maafisa wamesema. Waziri wa sheria wa Jimbo la Jonglei, Gabriel Duop Lam aliambia BBC kuwa takriban watu 200 wengine wamejeruhiwa.

Mwandishi wa BBC James Copnall, mjini Khartoum, anasema takwimu hizo zinaashiria kuwa kuna idadi kubwa zaidi. Wizi wa ng’ombe na mashambulizi ya kulipiza kisasi yamewaua maelfu ya watu tangu Sudan Kusini ijipatie uhuru wake mwaka 2011

Mwandishi wa BBC anasema mapigano yaliwahusisha makundi hasimu kutoka jimbo la Jonglei ambayo yanatokana na mzozo wa mpaka katika jimbo laUpper Nile.
Vijana wa kabila la Murle walivamia kamvi kadhaa za ng’ombe siku ya Ijumaa, maafisa wa eneohilowalisema.

Maelfu ya ng’ombe inaripotiwa kuibiwa yakilenga maeneo manane ya kaskazini katika ji wa Akobo. Gavana wa jimbo la Jonglei Kuol Manyang aliiambia BBC kuwa tau 100 waliuawa.

Mwezi Januari mamia ya watu wa kabila la Murle waliuawa Jonglei kwa nguvu ya wapiganaji 6,000 hasa kutoka kundi hasimu la kabila Lou Nuer. Maelfu ya watu wa kabila la Murle wamekimbia makwao baada ya mashambulizi kama kisasi kwa mauaji ya watu 600 mwezi Agosti mwaka 2011.

Kabila la Murle na la Lou Nuer yana historia ya kuibiana ng’ombe mara nyingi yakianzisha ghasia. Majeshi ya Sudan Kusini na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamesema watatuma vikosi zaidi katika jimbo la Jonglei kudhibiti mashambulizi.
-BBC