Serikali yamaliza mgogoro wa Ndanda Sec.

Naibu Katibu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Selestine Gesimba (katikati) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu makubaliano baina ya Serikali na Viongozi wa Taasisi za Kiislamu kuhusu mgogoro wa shule ya Sekondari Ndanda iliyoko Masasi mkoa wa Mtwara leo jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine serikali itawarudisha shuleni mwaka huu wanafunzi wote 62 waliohusika na mgogoro wa shule hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Sheikh Musa Kundecha, Amir wa Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania na Bw. Samweli Kusaga kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Idara ya Sekondari.

Viongozi wa Taasisi za Kiislamu Tanzania wakiongozwa na Sheikh Musa Kundecha (pili kutoka kulia) ambaye ni Amir wa Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania wakijadili jambo na Rais wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA) Jaafar Mneke (katikati) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliojadili makubaliano baina ya Serikali na Viongozi wa Taasisi za kiislamu kuhusu mgogoro wa Shule ya Sekondari Ndanda.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndanda waliosimamishwa masomo kufuatia mgogoro wa shule hiyo wakifuatilia tamko la makubaliano ya viongozi wa dini ya kiislamu na Serikali lililotolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Selestine Gesimba kufuatia mkutano wa pamoja uliofanyika tarehe 7 mwezi huu.