Meneja Mahusiano kwa Umma na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akionesha nambari za washindi 100 wa droo ya siku ya promosheni ya M-PESA waliojishindia sh. 50,000 kila mmoja. Wanaoshuhudia ni Mtaalamu wa Huduma za Ziada kwa Wateja wa Vodacom, Bi. Reenu Verma na Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid. Droo hiyo imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Bakari Maggid akirekodi taarifa za washindi 100 wa droo ya siku ya promosheni ya M-PESA waliojishindia sh. 50,000 kila mmoja baada ya kuchezeshwa na Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom Bi. Reenu Verma (katikati) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mahusiano kwa Umma na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu.