WATETEZI haki za wanyama wameiomba Misri na Djibouti zikubali meli yenye matatizo na iliyosheheni maelfu ya ng’ombe itie nanga katika bandarini moja wapo.
Shirika liitwalo “Huruma kwa Wanyama” linasema kuwa limepata taarifa kuwa ng’ombe karibu 3,000, waliopo kwenye meli hiyo ya Gracia del Mar, wameshakufa.
Meli hiyo imetia nanga kwenye Bahari ya Sham, tangu ilipopata matatizo kwenye mitambo na imekataliwa kushusha mali katika nchi iliyokuwa ikielekea, yaani Misri.
Meli hiyo ilianza safari yake Brazil, majuma kadha yaliyopita. Haijulikani kwanini ilizuwiliwa kuingia bandarini, nchini Misri.
-BBC