RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dk. Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango (MARCO).
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Peniel Lyimo Februari 2, 2012, Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Februari 20, mwaka huu wa 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Dk. Rutasitara alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.