ZAO la muhogo linaweza kusaidia wakulima wa Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, taarifa za wanasayansi zinasema.
“Ni zao linalostahamili ukame kuliko mazao yote ya chakula,” amesema Kiongozi wa ripoti, Andy Jarvis, wa Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo ya nchi za joto, Colombia.
“Wakati mazao mengine makuu yanaweza kuangamizwa na joto na matatizo mengine ya mabadiliko ya tabia nchi, muhogo unaweza kustahimili.” Amesema, Andy Jarvis.
Zao hilola mzizi tayari linatumika zaidikamachakula kikuu barani Afrika.
Lakini ripoti hiyo imesisitiza kuwa inahitajika utafiti zaidi ili kuufanya muhogo kupambana na wadudu na magonjwa.
Mwezi Novemba uliopita wanasayansi walionya kuwa virusi vingevamia zaohilona kulifanya janga katika baadhi ya sehemu za Afrika. Athari za virusi zimekuwa zikikumba baadhi ya maeneo yanayokabiliwa na njaa.
Chanzo cha zao hilo ni Amerika Kusini, muhogo uliletwa katika Sfrka kusini mwa jangwa laSaharana wafanya biashara wa Kireno katika karne ya 17. Likakua katika udongo usio na rutuba na wenye maji kidogo.
Kwa mujibu wa watatfiti wa ripoti hiyo inayosema ‘Je muhogo ni jibu la kutegemewa katika mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika? Sasa ni chanzo cha pili muhimu cha upatikanaji wa wanga barani humo huku likitumiwa na watu akribu milioni 500 kila siku.
Muhogo unayapita mazao mengine sita ambayo yanatumiwa barani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara-viazi, mahindi, maharage, ndizi, mtama na uwele-katika vipimo sita vya utabiri wa mabadiliko ya tabia nchi 24, ripoti inasema.
Zao hilo linakuwa vizuri katika eneo lenye joto zaidi na iwapo ukame unatokea, linajifunga mpaka mvua itakaponyesha tena, wanasayansi wanasema.
“Tuna hadithi nzuri chache ambapo tunaona mazao yanayolingana na mazuri katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na hatimaye tukaona muhogo ndio wenye ” Bw Jarvis alikiambia kipindi cha BBC- Network Africa
Alisema hizi ni habari njema kwa Afrika, hasa Nigeria taifa linalolima muhogo kwa wingi Afrika, huku likilima tani “£36-37 mega (million) za zao hilo kwa mwaka”, na Jamhuri ya Kidemokrasi yaCongoikishika nafasi ya pili.
Muhogo unaweza kuwa zao mbadala sasa wakati mazao mengine yameshindwa “, Bw Jarvis alisema.
“Kwa Afrika Mashariki mahindi yanapendelewa zaidi na wakulima wengi na muhogo unaweza kuwa zao mbadala-zao la pili mbadala.”
Mzizi huo wenye wanga mwingi unalimwa kwa kiasi kidogo tu Kusini mwa Afrika, ambako kuna hali ya hewa baridi wakati wa mwezi wa baridi. Lakini hii inaweza kubadilika.
Katika taarifa, aliongeza: “Kwa matumaini, utafiti huu utakwenda sambamba na na wito kwa jamii ya wanasayansi kubadili mitazamo yao kuhusu.”
-BBC