Na Mwandishi Wetu
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata bunduki mbili, risasi 93 pamoja na watuhumiwa 313, katika kipindi cha Januari na Februari kufuatia msako mkali wa kupambana na uhalifu ulioendeshwa jijini hapa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema operesheni hiyo ya polisi imekamata silaha mbili aina ya shortgun pamoja na risasi 93.
Aidha Kamanda Kova amesema takwimu za mwezi Januari na Februari zinaonesha kupungua kwa matukio ya uhalifu jijini Dar es Salaam ikilinganishwa na miaka mingine, huku akiwata watu wanaotoa taarifa ambazo si sahihi kwa polisi kuacha mara moja kwani zinawatia hofu wananchi.
Pamoja na hayo, amewashukuru wananchi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kufanikisha msako huo na kuwapongeza wote wanaoitaarifu polisi ili kudhibiti uhalifu.