RAIS mpya wa Yemeni, Abd-Rabbu Mansour amenusurika kulipuliwa na bomu baada ya bomu kubwa lilotegwa kwenye gari, nje ya nyumba yake, Kusini mwa Yemen, mjini Mukalla, kulipuka na kuuwa watu wapatao 20.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema shambulio limefanywa wakati rais mpya Abd-Rabbu Mansour Hadi akiapishwa. Rais huyo amechukua kiti cha Ali Abdullah Saleh, ambaye ameongoza nchi kwa miaka 33.
Abd Rabo Mansour Hadi aliapishwa rasmi, baada ya uchaguzi uliofanywa Jumane, ambapo hakuwa na mpinzani. Hiyo ilikuwa sehemu ya makubaliano, ambayo yanampa idhini huyo makamo wa rais wa zamani, kusimamia shughuli za kutayarisha katiba mpya, na kipindi cha mpito cha kuelekea kwenye demokrasi.
Rais mpya aliahidi kushughulika ili Wayemeni waweze kurudi majumbani mwao…baada ya kuhama kwa sababu ya mapambano nchini humo. Na aliahidi kuendelea kupambana na Al Qaeda, ambayo ina wafuasi nchini Yemen.
Wakati anaapishwa, bomu lilotegwa kwenye gari liliripuka na kuharibu nyumba ya rais, kusini mwa nchi, na kusababisha vifo vingi na majaraha. Matatizo ya Yemen ni mengi, na siyo ya ugaidi tu. Nchi hiyo imegawanyika kikabila na kidini.
Pato lake kubwa linatokana na mafuta, ambayo yanapungua haraka. Na Yemen ni nchi ambayo inatabiriwa kuwa ya mwanzo kuishiwa na maji.
-BBC