WAPIGANAJI sita wa kigeni kutoka kundi la Kiislamu la Al-Shabaab wameuawa kwenye shambulio la anga lililotekelezwa Kusini mwa Somalia. Walioshuhudia tukio hilo wanasema, watu 6 waliuawa wakiwemo raia kadhaa wa kigeni.
Magari mawili yaliharibiwa wakati wa shambulio hilo la anga lililofanyika katika eneo linalojulikana kama K60 takriban 60km kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
Taarifa zilizoripotiwa na BBC mjini Mogadishu, zinasema mlipuko huo ulisikika umbali wa 150 km. Hivi majuzi kundi la Al-Shabaab, lilitangaza kuwa linajiunga na kundi la al-Qaeda na inasemekana kundi hilo linajumuisha wapiganaji 200 wa kigeni.
Kufikia sasa haijulikani nani aliyetekeleza shambulio hilo, lakini mwandishi wetu anasema shambuliuo hilo ni kubwa zaidi kuliko shambulio lolote ambalo limewahi kutekelezwa na wanajeshi wa Kenya KDF, ambao wako maeneo ya Kusini mwa Somalia.
Wajeshi wa Marekani wmefanya mashambulio kadha dhidi ya wapiganaji wa al_Qaeda nchini Somalia. Hapo jana Waziri mkuu wa nchi hiyo alitaka jamii ya kimataifa kufanya mashambulio zaidi ya anga dhidi ya wapiganaji hao wa al-Shabab.
Waziri huyo mkuu alikuwa akizungumza katika mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia uliokuwa umeandaliwa mjini London, kutafuta mbinu za kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Somalia uliodumu kwa zaidi ya miongo miwili.
-BBC