KUMBUKUMBU
NI miaka 23 sasa tangu umetutoka lakini watoto wako pamoja na Baba uliyetuachia tunaona ni kama jana tu umeondoka, maana umeenda kimwili lakini kiroho bado tupo nawe, na kamwe hatutaacha kukumbuka malezi yako bora uliotupa!
Tukiwa kama familia (watoto wako pamoja na mumeo (Baba) daima hatutakoma kukuombea DUA njema kila kukicha upate kupumzika kwa amani huko uliko.
Ni matumaini yetu Mungu anasikia dua zetu MAMA
Ni sisi wanao wapendwa Mariam, Hussein, Salum, Mariam Hawa pamoja na Baba yetu (mumeo) Sheikh Suleiman. Hatuna la zaidi ila ni dua tunakuombea,
“INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAAJIUN”