Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (wa pili kulia) akifuatana na Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, pia Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Haji Omar Kheri, pamoja na viongozi wengine wakielekea katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani, kuhudhuria katika Sherehe za uzinduzi wa Maulid ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W), mara baada ya kuwasilimkatika kisiwa cha Tumbatu.
Baadhi ya akina Mama waliohudhuria katika hafla ya upandishwaji wa Bendera, wakati wa Uzinduzi wa sherehe za Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) wakifuatilia hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, zilizofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tumbatu Gomani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (wa nne kushoto) pamoja na Viongozi wengine walipohudhuria katika hafla ya upandishwaji wa Bendera wakati wa Uzinduzi wa sherehe za Maulidi ya kuzaliwa kwa Nabii Muhammad (S.A.W) mbele ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.
Sheikh Othman Maalim akitoa Mawaidha ya Kiislamu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad S.A.W zilizofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani, yaliyohuduriwa na waislamu wa Shehia za Tumbatu na Vijiji jirani. (Picha zote na IKULU).