RAIS Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Erastus Mwencha, Naibu Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika. Katikati ni Kamishna wa Maendeleo ya vijijini na Kilimo wa Kamisheni hiyo, Bi Rhoda Tumusiime waliomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Januari 16, 2012. Viongozi hawa wako nchini kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Kilimo toka nchi Saba za Afrika unaofunguliwa leo Januari 17, 2012 Kilimanjaro Hyatt Hotel jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.