Na Mwandishi Wetu
WAKATI mwingine mtu unaweza kuwa na wazo zuri la kimaendeleo lakini baada ya kulitekeleza na usimamizi wake kuwa mbaya laweza onekana kero kwa wahusika. Hali hii ipo kwa wafanyabiashara wanaotumia Soko Maalumu la Wafanyabiashara Ndogo ndogo (yaani Machinga Comlex) la jijini Dar es Salaam.
Jengo hili kubwa ambalo lilijengwa kwa fedha nyingi kwa ajili ya Wafanyabiashara Wamachinga sasa halitumiki ipasavyo au kama ilivyotarajiwa na limekuwa likiwapa machungu na hasara kubwa wafanyabiashara waliokubali kupanga katika soko hilo.
Wafanyabiashara hao hawapati wateja katika biashara zao kutokana na soko lililotazamiwa kuamia eneo hilo kushindwa kufanyika. Kutokana na mgawanyiko huo baadhi ya wafanyabiashara wachache walikuja eneo la soko baada ya kukamilika, lakini walipobaini wenzao wamegoma kuhama maeneo ya awali baadhi nao wakarejea kule na kuancha soko hilo.
Sasa walioingia mkenge na kuhamia katika soko hilo hawapati wateja kabisa kwa kile wengi wa wateja bado wanapata huduma zao kule kwenye soko la zamani. Hata hivyo eneo lilipojenga viongozi wameshindwa kuweka miundombinu ya kuwavuta wateja eneo hilo, sasa limekuwa kama kisiwa. Hakuna wateja kabisa utadhani ni stoo ya wafanyabiashara. Hebu angalia picha hizo uone hali halisi baada ya mwandishi wa mtandao huu kutembelea hapo leo.