Na Mwandishi Wetu, Arusha
HAPPY Kivuyo ambaye ni shahidi wa tatu kesi namba 13 ya 2010 ya kupinga matokeo ya ushindi Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amedai mahakamani kuwa alimsikia mbunge Lema katika mikutano yake ya kampeni akiwashawishi wapiga kura kumchagua ili aiondoe madarakani Serikali ya majambazi.
Shahidi huyo alitoa madai hayo jana mbele ya Jaji Gabriel Rwakibarila wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, wakati alipokuwa akiongozwa na Wakili, Alute Mughwai. Alidai kuwa Lema alitoa kauli hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Cheka ung’atwe, lililopo Kata ya Sombetini Oktoba 2 mwaka 2010.
“Lema alisema kuwa Arusha inahitaji kiongozi jasiri kama yeye ili Serikali ya majambazi iondoke madarakani,” alidai shahidi huyo. Happy aliieleza pia kuwa Lema akiendelea na mkutano huo, alikuja Mwana CCM mmoja aliyemtaja kwa jina la Justine Koikai ambapo alidai Lema alimwambia kuwa “nakushangaa rafiki yangu unaendelea kung’ang’ania CCM, hivi unajfahamu wenye CCM wenye CCM wanatembea na VX huku wewe ukiwa unatembea na namba 11(miguu)”alimnukuu Lema shahidi huyo.
Aliongeza kuwa Lema aliwaambia watu waliokuwa katika mkutano huo kuwa, tangu lini waarusha wakaongozwa na mwanamke? kazi ya mwanamke ni kukaa jikoni siyo kuongozwa Malaigwanan,” Ningejua Batilda ndiye anagombea mimi nisingegombea ningemleta mke wangu kwa sababu huyo (Batilda0 siyo saizi yangu” alimnukuu Lema.
Aidha katika hatua nyingine shahidi huyo alijikanganya mahakamani hapo baada ya kutoa maelezo tofauti wakati alipouwa akihojiwa na Wakili wake na wakati alipokuwa akihojiwa na wakili wa mdaiwa wa kwanza Method Kimomogolo.
Awali Shahidi huyo akiongozwa na wakili wake, aliieleza mahakama kuwa wakati anakwenda kwenye mkutano huo ambao ulikuwa unafanyika karibu na nyumbani kwake majira ya saa 10 jioni, alikuwa amewaacha wageni nyumbani kwake ambao walikuwa wamepeleka posa.
Aliseman kuwa wakati akiwa katika mkutano huo, mtoto wake alikwenda kumuita kwa sababu wageni aliokuwa amewaacha nyumbani kwake walipata vinywaji na chakula walikuwa wanataka kuondoka. Akihojiwa na Wakili Kimomogoro, Happy aliieleza Mahakama kuwa wakaatika akiwa katika mkutano huo wa kampeni, mtoto wake alikwenda kumuita kwani nyumbani, wageni ambao walikuwa wamefika hapo kwa ajili ya kupeleka posa, walishafika.
Hoja iliyokuwa inabishaniwa hapo ilikuwa ni lipi sahihi kati ya kuwa alikwenda kwenye mkutano kabla ya wageni hao kufika au baada ya wageni kufika.
Mahojiano kati ya Shahidi huyo na Kimomogoro yalikuwa hivi:
Wakili: Haya maneno ya uliyosema hapa ukidai Lema aliyasema wakati wa
kampeni kuwa kazi ya mwanamke ni kukaa jikoni na siyo kushika
madaraka, mbona hayapo kwenye hati ya madai?
Shahidi: Sijui ila wakili kazi yake kuandika kama aliyaacha sijui
Wakili: Nakuuliza tena haya maneno yapo katika hati
Shahidi: Nilimweleza mwanasheria wangu yeye anajua
Wakili: mliwahi wewe na wenzako kuomba kibali cha mahakama hii ili
kuruhusu kufungua kesi hii
Shahidi: kazi hiyo tulimwachia mwanasheria wetu
Aidha shahidi huyo alipoulizwa kama aliwahi kuwa kiongozi wa ngazi
yoyote ndani ya CCM alisema kuwa aliwahi kuwa Katibu Hamasa katika
Kata ya Sombetini kw akipindi cha takribani miaka (3) ila alidai
kuenguliwa baada ya kuhitilafiana na viongozi wenzake.
Aliieleza Mahakama hiyo kuwa uongozi wa halamashauri KUU ya CCM katika
kata hiyo walipomvua madaraka Juni 2010 walimkataza kujihusisha na
shughuliz aCCM ndani ya hiyo kata ambapoi hadi hivi sasa anatumikia
adhabu hiyo. Alidai mahakamani hapo kuwa chanzo cha yeye kufukuzwa ni baada ya kumkataa aliyekuwa mgombea wa udiwani kupitia CCM Calisti Lazaro kwa
madai alikuwa pandikizi la CHADEMA, huku baadhi ya viongozi wenzake
wakimuunga mkono aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo. Jaji Rwakibarila aliahirisha shauri hilo hadi leo ambapo shahidi wa nne anatarajiwa kutoa ushahidi wake