Tamasha la Vodacom ‘Shuffle Dance’ Dar

Wasanii mbalimbali na vijana waliojitokeza kushiriki Tamasha la Vodacom ‘Shuffle Dance’, wakicheza staili moja kwa pamoja wakati wa Tamasha hilo lililofanyika juzi kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam, Tamasha hilo likiwa na lengo la kuvunja na kuweka rekodi ya Dunia katika kitabu cha Matukio Makubwa yanayotokea duniani, ‘Guinness Book Records’. Tamasha liliandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

Picha nyingine inaonesha helkopta ikipita kandokando ya Bahari ya Hindi eneo la Ufukwe wa Sunrise Resort juzi, wakati wa Tamasha la Vodacom la ‘Shuffle Dance’, lililoandaliwa maalum na kampuni hiyo ya Vodacom kwa ajili ya kuweka na kuvunja rekodi ya dunia na kuweka kumbukumbi katika kitabu cha Matukio makubwa Duniani ‘Guinness Book Records’.Tamasha hilo lilifanyika juzi (Ijumaa) kwenye Ufukwe wa Hotel ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam. (Picha zote kwa hisani ya Vodacom Tanzania)