Mkataba wa vijana bungeni leo-Mnyika

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika

*Tip za Mnyika bungeni

KWA Vijana wenzangu kwa nafasi na wote wenye nafsi za ujana, leo ule mkataba wetu wa Afrika (African Youth Charter) hatimaye unaingia bungeni kuridhiwa. Ni matokeo ya harakati zetu za miaka mingi kabla na hata baada ya Rais Kikwete kuusaini Gambia mwaka 2006 lakini ukaishia makabatini. Baada ya kunituma bungeni kuwatumikia mkataba huu ni kati ya mambo niliyohoji mara kwa mara kutaka uletwe bungeni kuridhiwa ili utekelezaji wake uweze kuanza.

Nawashukuru wote tuliounganisha nguvu kwenye harakazi za vijana kwa nyakati mbalimbali kuanzia NYF, TYVA, YUNA, TSNP, UDSM, BAVICHA, asasi zingine na mwisho lakini kwa umuhimu mkubwa vijana wote tuliokesha pamoja kulinda kura Loyola.

Kwa kurejea nyuma katika historia, nawaletea moja ya ujumbe nilioandika kwenu na kwa vijana wa Afrika mwaka 2008: http://mnyika.blogspot.com/​2008/10/​vijana-tufikiri-na-kuungana-kuk​omboa.html Kila kizazi lazima kiitambue dira na dhima yake; ama kisaliti au kitimize. Tuendelee kuwajibika; kwa pamoja tunaweza.