Bia ya Serengeti katika muonekano tofauti, ladha ile ile

Bia ya Serengeti kama inavyoonekana katika muonekano mpya baada ya kuzinduliwa. Hata hivyo ladha na ubora ni ule ule wa awali. Bia hiyo inazalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Tanzania. Picha na Joachim Mushi)


Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL), Ephraim Mafuru akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Serengeti katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Na Joachim Mushi

BIA maarufu ya Serengeti inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti nchini (SBL) jana usiku imezinduliwa katika muonekano mpya huku ikibaki na ladha na ubora ule ule wa awali. Hafla ya uzinduzi wa muonekano huo mpya wa bia ya Serengeti umezinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi. Joyce Mapunjo katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Mapunjo amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa kampuni ya Bia ya Serengeti katika kukuza na kuendeleza uchumi wa Taifa, hivyo kuwataka wawekezaji wengine kufuata nyayo za SBL.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Richard Wells (kulia) akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa Bia ya Serengeti jana.


Alisema Serengeti ni moja kati ya kampuni zilizojenga historia kubwa ya mafanikio katika sekta binafsi, jambo ambalo limekuwa na mvuto. “Hakika leo sote tunakiri na kushuhudia mafanikio makubwa katika kampuni hii ingawa kuna makampuni mengi makubwa ambayo yanatengeza bidhaa na kuleta ushindani katika soko la kimataifa,” alisema Katibu huyo Mkuu mwenye dhamana ya biashara nchini.

“Bidhaa kama hii tuliyoshuhudia uzinduzi wake leo, sisi ni mashahidi kuwa bidhaa hii ni nzuri na hakika itavuka mipaka na kufikia masoko yaliyo nje ya mikapaka yetu, siku zote nimekua nikiitaja kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuleta mabadiliko kwa bidhaa bora ambayo inaleta changamoto ya biashara na furaha ya kipekee kwa wateja wake,” aliongeza Mapunjo.

Mfano wa chupa kubwa ya Bia ya Serengeti ukiibuka ndani ya machi wakati wa hafla ya uzinduzi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru alisema kuwa pamoja na muonekano mpya wa bia ya Serengeti sasa bado imebaki na ladha yake ya kipekee na ubora uliotukuka hivyo kuwaomba wateja waendelee kufurahia fahari hiyo.

“Bia ya serengeti inajulikana kwa ubora na ladha yake na imeshinda medali za dhahabu katika ngazi za kimataifa kama kama vile DLG & Monde pia ni bia ya kwanza Tanzania inayotengenezwa na kimea kwa asilimia mia moja. Bia ya Serengeti imejijengea historia kubwa katika nyanja mbalimbali hasa katika ujazo na thamani yake. Muonekano mpya bia wa Serengeti unavutia kwa wateja wwtu wa jinsia zote,” alisema.

Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Richard Wells, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bi. Joyce Mapunjo na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wakizungumza huku wakiendelea kufurahia muonekano mpya wa Bia ya Serengeti jana katika uzinduzi huo. Bi. Mapunjo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.


Aidha alisema kwa sasa bia hiyo uonekano huu mpya wa bia hii unajumuisha chata mpya na muonbado ina muonekano wa dhahabu unaoendana na staili mpya ya maisha ya kisasa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Richard Wells alisema SBL ambayo ni kampuni tanzu ya Diageo inazingatia sana ubora wa bidhaa zake, ikiwa ni pamoja na kuzizalisha kwa kutumia vimeng’enyo vya hali ya juu na katika mazingira safi na salama.

“SBL tunatumia bidhaa hasa zinazopatika ndani ya nchi yetu hivyo tunaamini pia kuwa tunachangia pato la taifa letu na ukuaji wa kilimo nchini. Pia mbali na uzalishaji huo tumekuwa tukiwajali wanajamii wanaotuzunguka kwa kujishughulisha na huduma muhimu za jamii.

“Tumechangia katika maeneo mbalimbali kuwapatia maji safi na salama, kuwajengea maarifa ya maisha wananchi, afya na mazingira. Tumejenga Hospitali ya Macho mjini Moshi, na tumepanda miti katika mikoa mbalimbali nchini kwa ushirikiano na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) na kudhamini wanafunzi kadhaa wanaofaulu na kushindwa kulipa ada,” alisema Wells.

Zaidi ya wageni waalikwa 200 kutoka sehemu mbalimbali nchini, wakiwemo wateja wa Bia ya Serengeti, wadau, pamoja na waandishi wa habari wameshuhudia hafla ya mwanzo ya tafsiri na muonekano mpya ya Bia ya Serengeti.
Uzinduzi huo wa aina yake uliosindikizwa na burudani kibao ikiwemo Bendi maarufu ya Extra Bongo ya Dar es Salaam ulitanguliwa na tafrija katika ukumbi mashuhuri ndani ya Hoteli ya Golden Tulip.