Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika jengo jipya la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga jana Januari 26, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Viongozi wa Wilaya ya Korogwe, wakikagua jengo la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Korogwe baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo hilo alipokuwa kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya wilaya hiyo jana Januari, 26, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa Mpunga kuhusu kilimo hicho cha umwagiliaji wakati alipotembelea na kukagua mashamba ya Skim Mamlaka ya Mji wa Mombo jana Januari 26, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma ujumbe ulioandikwa na vijana wa Harakati ya Mazingira, wakati akiwasili kwenye uwanja wa Mamlaka ya Mji wa Mombo kwa ajili ya kuwahutubia wananchi, akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga, jana Januari26, 2012. Kulia kwake ni mkewe Mama Zakhia Bilal na (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa. Picha na Muhidi Sufiani-OMR