Wadau wa mazingira wajadili mabadiliko ya tabia nchi

Mshauri wa masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID) nchini Tanzania Bi. Magdalena Banasiak (kushoto) akizungumzia athari za mabadiliko ya Tabia nchi duniani na mchango wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zilizoanza kujitokeza zinadhibitiwa. Picha na Aron Msigwa–MAELEZO.

Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akiwasilisha mada kuhusiana na mabadiliko ya Tabia nchi na ripoti ya tafiti ya athari za kimazingira iliyofanyika katika baadhi ya maeneo yakiwemo Zanzbar, Mbeya, Tanga, Manyara, Shinyanga na Mwanza leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Wadau wa Mazingira kutoka, Taasisi mbalimbali,wizara na wadau wa mazingira kutoka nchi wahisani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano unaojadili Mkakati wa Kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.