Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
TAARIFA ambazo zimetufikia ni kwamba mama mmoja (55) akiwa mtupu, yaani kama alivyozaliwa amedondoka kutoka angani alipokuwa akisafiri na ungo pamoja na mwanaye anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 9.
Watu hao wanaoshukiwa kuwa washirikina wamedondoka usiku wa kuamkia leo eneo la Vikindu, Wilaya ya Mkuranga nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Shuhuda wa tukio hilo ameueleza mtandao huu kuwa watu hao wamedondoka kwenye makazi ya mkazi mmoja usiku wa manane na baada ya kubainika wanakijiji wameamua kuwapeleka katika kituo kidogo cha Polisi eneo la Vikindu.
“Baada ya kuwakamata tumekubaliana tuwapeleke kituo cha Polisi Vikindu Usiku huo huo nadhani leo watapelekwa katika Kituo cha Polisi Mkuranga kwa hatua zaidi…kama unataka taarifa zaidi wasiliana na Polisi Mkuranga utapewa,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo alipohojiwa na mtandao huu.
Mtandao huu unaendelea kufanya mawasiliano na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga kupata ufafanuzi juu ya taarifa hizi.