Man City yaendelea kupaa, Man U yaifanyia vibaya Arsenal

Mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli

MSHAMBULIAJI, Mario Balotelli amejitokeza kuwa kiini cha mgogoro na sababu ya kuipatia ushindi Manchester City ikipiga hatua dhidi ya mshindani wake wa karibu Manchester United.

Balotelli aliingia wakati Manchester City ikisukumwa na Tottenham 2-2 baada ya kurudisha mabao mawili katika kipindi kifupi ikionekana kuondoka na angalau pointi moja.

Wakati ikionekana kua Manchester City imepungukiwa na maarifa Bario Balotelli aliangushwa ndani ya eneo la hatari na beki Ledley King na mshambuliaji huyo kufunga bao la City na kuiweka Spurs nyuma ya viongozi wa Ligi kwa tofauti ya pointi nane.

Habari kubwa kutoka mchuano huo hata hivyo haukua ushindi wa City bali gumzo lilizunguuka jinsi Balotelli alivyomkanyaga kichwani Scott Parker.

Harry Redknap aliwambia wandishi habari kua alishangazwa na jinsi refa alivyoshindwa kuliona kosa la Balotelli akimkanyaga Parker makusudi. Hivyo, Balotelli akaongezea umaarufu wake kwa mashabiki wa klabu yake wanaompenda licha ya wengi kuhusu ni juha katika soka ya England.

Manchester United imezidi kuipa shinikizo Manchester City iliyo kwenye kilele cha Ligi Kuu ya England kufuatia mkwaju wa Danny Welbeck dakika chache kabla ya mechi kumalizika. Mwanzoni mwa mechi hii United ilikua nyuma kwa pointi sita baada ya Manchester City kuirarua Tottenham hotspurs 3-2 kwenye uwanja wa Ettihad mapema siku ya Jumapili.

Manchester United iliongoza kwa bao la Antonio Valencia dakika moja kabla ya kipenga cha mapumziko kuipa klabu yake bao 1-0. Bao hilo lilifutwa na nahodha wa Arsenal katika kipindi cha pili na kuonekana kama liliowaamsha wachezaji wa Arsenal.

Mabadiliko yaliyofanywa na pande hizi mbili hayakuonekana kubadili mchezo ingawa wadadisi wengi wanajiuliza sababu iliyomfanya Arsene Wenge kumuondoa mchezaji wake aliyeonyesha mchezo mzuri Alex Oxlade-Chamberlain.

Licha ya juhudi na kuonesha matumaini ya kuongezea mabao kwa Arsenal Manchester United ikitumia uzowefu wake na kuzingatia mpango wake waliokuja nao waliendelea kuizuia Arsenal isifurukute na kama ilivyo tabia yao ya kukamilisha tamaa yao dakika za mwisho, zikisalia dakika tisa kabla ya kumalizika kwa mechi Danny Welbeck akatikisa nyavu za Arsenal na kuipatia ushindi na pointi tatu. Arsenal 1 Manchester United 2.
-BBC