Meli yapinduka Italia, yaua 3, abiria 50 wapotea

Sehemu ya Meli ya Costa Concordia ikiwa imezama upande mmoja

Meli ya Costa Concordia ikiwa imezama upande mmoja

VIKOSI vya uokoaji majini nchini Italia vimeanza kuikagua Meli ya Costa Concordia iliyopinduka upande mmoja baada ya kwenda mrama nje ya pwani ya magharibi Ijumaa usiku na kuuwa watu watatu.

Abiria wanasema walisikia kishindo kikubwa kabla ya meli hiyo, Costa Concordia, kutikisika na kusimama na taa kuzimika. Mlinzi mmoja wa pwani alisema inasadikika meli hiyo iligonga kitu ambacho kiliipasua meli upande wa kushoto.

Taarifa zaidi zinasema meli ilipoanza kuingia maji, kilipigwa king’ora kuwaonya watu watoke kwenye meli, na abiria na mabaharia zaidi ya 4000 walichupa majini na kuogelea hadi kisiwa cha Giglio kilioko karibu na eneo la ajali.

Inakadiriwa kuwa abiria takribani 50 hawajulikani walipo, japokuwa baadhi ya maofisa nchini Italia wanasema huenda orodha ya abiria waliopo kwenye meli ikawa na upungufu wa taarifa.

Meli hiyo kubwa ya kifahari nchini humo inayofanya safari majini maeneo kadhaa inasadikiwa ilikuwa abiria wengi ni raia wa Italia, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.
-BBC