Wilson Mukama awa Katibu Mkuu CCM

Katibu Mkuu mpya wa CCM, Wilson Mukama

HATIMAYE kitendawili cha mageuzi mkubwa ya CCM kupata viongopzi wapya wa Kamati Kuu (CC) ya Chama hicho kimeteguliwa na sasa atakayeshika nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa ni Wilson Mukama, huku akisaidiwa na John Chiligati kama Katibu Msaidizi aliyekuwa mwenyekiti Itikadi na Uenezi wa uongozi uliojiuzulu.

Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Nape Mnauye, anaye kuwa Katibu wa Itikadi na Habari, January Makamba anayekuwa Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje wa CCM, Lameck Nchemba Mweka Hazina mpya, Asha Abdullah Juma anayekuwa Katibu Oganaizesheni, Vuai Ali Vuai anayeshika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Wajumbe wengine wanaoingia Kamati Kuu ya CCM ni Pindi Chana, Abdulrahiman Kinana, Zakhia Meghji, Abdullah Kigoda, Steven Wasira, Costansia Buhiye, William Lukuvi, Dk. Hussein Mwinyi, Dk. Maua Daftari, Samia Suluhu, Shamsi Vuai Nahodha, Omarry Yusufu Mzee, Prof. Makame Mbarawa, na Mohamed Khatibu.