MASENETA wa chama cha Republican nchini Marekani wamepinga pendekezo la kuwaruhusu wapenzi wa jinsia moja kuhudumu wazi katika jeshi la Marekani.
Wamedai kuwa uwezo wa jeshi utavurugwa na kurudisha nyuma sera zilizopo zinazofahamika kama ‘Usiulize,Usiseme.’
Maseneta wawili wa chama cha Democrat waliungana na wale wa Republican kutupilia mbali mageuzi ambayo yaliungwa mkono na rais Obama.
Rais Obama alipigia debe mabadiliko ya sheria hiyo na kura ya maoni inaonyesha kuwa wengi wa raia wa Marekani wanamuunga mkono.
Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Washington anasema ni suala la kisiasa na wengi wa wabunge wa Demokrat katika seneti walilipigia kura ya ndio sawa na wale wa Republican.
-BBC