Walioibia majibu Std VII kurudia mtihani Septemba

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo (kushoto) akitoa tamko leo jijini Dar es Salaam kuhusu hatma ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011 ambapo Serikali imeamua watahiniwa 9,629 waliofutiwa matokeo kutokana na kubainika majibu yao kufanana kurudia mtihani wa darasa la Saba mwezi Septemba mwaka huu 2012. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Elimu ya Msingi, Zuberi Samataba.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo (katikati) akitoa tamko leo jijini Dar es Salaam kuhusu hatma ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011 ambapo Serikali imeamua watahiniwa 9,629 waliofutiwa matokeo kutokana na kubainika majibu yao kufanana kurudia mtihani wa darasa la Saba mwezi Septemba mwaka huu 2012. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Elimu ya Msingi, Zuberi Samataba (kulia) na Mkuu wa Idara ya Elimu ya Sekondari na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Charles Philemon(kushoto) Picha zote na Tiganya Vincent- MAELEZO, Dar es Salaam.