Na Janeth Mushi, Arusha
AMANI ya Tanzania inaweza kulindwa na kudumishwa endapo viongozi wa Serikali na vyama vya siasa watatimiza wajibu wao na kuhimiza wananchi kuwa wazalendo na kutenda.
Changamoto hiyo imetolewa hivi karibuni mjini hapa na Mchungaji Andrea Kanjembe wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mt. Kilimanjaro DMK Prisha ya St. James wakati alipokwua akifungua mkutano ulioshirikisha Chama Cha waandishi wa habari mkoani hapa Arusha Press Club (APC) na wadau mbalimbali wa habari.
“Huwezi kulazimisha amani ya nchi kwa kutumia bunduki ila watu
wakihimizwa kuwa wazalendo, haki ikitolewa bila kulazimishwa amani
itakuja kama mwangaza,” alisema
Aidha mkutano huo ulioandaliwa na Umoja wa vyama vya waandishi wa
habari nchini (UTPC) uliokuwa na lengo la kuwakutanisha na wadau wa
habarikujadili mambo yanayohusiana na habari, changamoto na namna ya kuzikabili. Mchungaji huyo alisema kuwa wakati taifa limetimiza miaka 50 ya Uhuru, maadili kwa viongozi lazima yazingatiwe.
“Msitaje amani kabla ya uzalendo, kabla ya uzalendo na haki, miaka ya 1960 viongozi walikuwa na uzalendo na taifa, tendeki haki damu
isimwagike kwa sababu ya madaraka na kusababisha tuuane sisi kwa
sisi, kwani kiongozi anayeongoza mkoa wa Arusha anatakiwa kuwa makini kwani Arusha ni mkoa mdogo ila una mambo magumu,” alisisitiza mchungaji huyo. Kiongozi huyo aliwataka waandishi wa habari kutambua kuwa wana nafasi muhimu sana katika jamii hivyo kuwasihi kuwa na hofu ya Mungu katika utendaji wao wa kazi.
Naye Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, aliwataka waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli wkani jamii inaamini yale yanayoandikwa katika vyombo vya habari.
“Matumizi mabaya ya kalamu ni zaidi ya jambazi mwenye bunduki na
risasi kwani mwandishi anayetumia kalamu yake vibaya na kutokusimamaia ukweli hususani kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 mambo mengi yatajitokeza kabla ya uchaguzi hivyo mnapaswa kuwa makini kwani mnayo nafasi kubwa kuibadilishwa taswira ya nchi,” alisema Lema.
Kwa upande wake Mkaribu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa
Peter Mvulla, alisema kuwa vyombo vya habari hapa nchini vimekwua
chachu ya kufichua maovu yanayoendelea ndani ya jamii.