Mji wa Sudan Kusini watekwa

RAMANI INAYOONYESHA MIPAKA YA NCHI YA SUDANI KUSINI

MJI wa Pibor ulitekwa na kabila la Lou Nuer Jumamosi, ingawa kulikuwa na askari wa Umoja wa Mataifa hapo pamoja na wanajeshi wa serikali.

Shirika la msaada wa matibabu la kimataifa, MSF, linasema kuwa lina wasiwasi mkubwa juu ya wafanyakazi wao zaidi ya 150 ambao wamekimbilia vichakani, wakati wa shambulio hilo, lilofanywa na maelfu ya watu wa kabila la Lou Nuer.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema nyumba pamoja na kanisa zilichomwa moto, na mali iliporwa.
Shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mashambulio yaliyofanywa na kabila la Murle katika miezi ya karibuni.
Msemaji wa MSF, Parthesarathy Rajendran aliiambia BBC, kwamba shirika hilo litaanza tena shughuli zake za kutibu watu, hali ikitulia tu.
Lakini alisema MSF kwanza inahitaji kutafuta watu wake, na kwamba inawasiliana na wale waliobaki eneo la Pibor.

-BBC