Bondia Super ‘D’ ajivunia mafanikio 2011

Aliyekuwa bondia wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila 'Super D'

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila ‘Super D’ na kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti ya Mkoa wa Ilala kimichezo amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata katika mchezo wa ngumi kipindi cha mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam Super ‘D’ alisema moja ya mafanikio hayo ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi
na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.

Alisema ameweza kushirikiana vema na wadau wa ngumi pamoja na mapromota mbalimbali wanaoandaa mapambano makubwa kwa kutoa
mchango wake wa vifaa vya ngumi ili kufanikisha mapambano mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka huu.

Katika hatua nyingine Super ‘D’ amekua akitoa mafunzo ya mchezo wa
ngumi pamoja na kutambua sheria mbalimbali kwa njia ya DVD
zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala ‘Super D’ kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khanny, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo
kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Alisema mipango yake kwa mwaka 2012 ni kuhakikisha anaendelea kuwainua mabondia wengine chipukizi akiwemo bondia Shomari Mirundi na Ibrahimu Class ambao amewataja ni mabondia wazuri wanaohitaji kuendelezwa vipaji vyao.

Alisema bondia Ubwa Salum ambaye alimtwanga Mustapha Doto, kwa pointi 60-57 alishinda ambapo pambano hilo lilikuwa moja ya mapambano ya utangulizi ya pambano kubwa la Rashidi Matumla na Maneno Osward lililofanyika Desemba 25 mwaka huu.

Mhamila mbali na kufanya kazi ya kuwanoa vijana katika mchezo wa ngumi pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha.