WATOTO wa Shirika la Utoto Mtakatifu wa Yesu Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana wamefanya misa kuwakumbuka mashahidi wa watoto waliouwawa miaka 2000 iliyopita wakati Mtoto na Mfalme wa ulimwengu Yesu Kristu alipozaliwa.
Misa hiyo maalumu iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Parokia ya Msimbazi Centre imeongozwa na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo kwa watoto wa Utoto Mtakatifu ni maalumu kwa ajili ya kuwakumbuka watoto waliouwawa na wafalme wenye uchu wa madaraka, waliokuwa na kusudi la kuuwawa kwa mtoto Yesu kipindi kifupi baada ya kuzaliwa.