Bondia Maneno Osward (kushoto) akimuacha Rashidi Matumla chini baada ya kuanguka kwa kuteleza wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Rashidi Matumla (kushoto) na Maneno Osward wakioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na superdboxingcoach.blogspot.com)
MPAMBANO kati ya mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ umemalizika jana jijini Dar es Salaam huku mabondia hao wakitoshana nguvu.
Katika pambano hilo lililokuwa na ushindani mkubwa lilimalizika huku mabondia wote wakiibuka na pointi 99 kwa 99, hivyo majaji kulazimika kutoa droo kwa wababe hao.