Mcheza kiungo wa klabu ya Manchester City na Timu ya Taifa ya Ivory Coast,Yaya Toure amechaguliwa kua mchezaji bora wa soka na Shirikisho la soka ya Afrika(CAF)
Mchezaji huyo mashuhuri alipitia mchujo wa ushindani na Seydou Keita kutoka Mali anayechezea klabu ya Barcelona na Andre Ayew wa Ghana pia klabu ya Olympique Marseille.
Toure, mwenye umri wa miaka 28, alichaguliwa na Makocha wa Timu za Mataifa ya Afrika kutoka nchi wanachama wa CAF.
Mwenyewe Yaya Toure alisema baada ya kutangazwa kua mchezaji bora kua, ”Hii ndio zawadi kubwa ambayo ningeweza kuipokea katika maisha ya uchezaji wangu soka.”
Inakumbukwa kua Yaya Toure ndiye aliyefunga bao pekee la klabu yake ilipoibwaga Stoke City katika fainali ya Kombe la FA mnamo mwezi Mei.
Toure aliyekua amebubujika kwa furaha alisema kua anajivunia tuzo hio na ni siku kuu kwake, na kuongezea kua ana imani hilo litaipa Timu yake ya Ivory Coast msukumo wakati wakiazimia kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika hapo mwakani.
Ushindi wa Toure ulihitimisha furaha ya nchi yake ya Ivory Coast ambayo ilikua tayari inasherehekea mshindi wa zawadi ya Refa bora wa CAF iliyomwendea Noumandiez Doue.
Mchezaji chipukizi aliyejitokeza ni mchezaji mchanga anayechezea klabu ya Tottenham, Souleyman Coulibaly aliyeshinda zawadi ya mchezaji bora mdogo mwenye kipaji. Oussama Darragi wa klabu ya Esperance akachaguliwa ,chezaji bora anayecheza soka yake barani Afrika kama mchezaji bora wa mwaka.
Kocha wa mwaka alikua Harouna Doula aliyeiongoza Timu ya Taifa ya Niger hadi kufuzu kwa fainali za fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huku Botswana nayo ilitajwa kama mojapo ya Timu zilizofuzu kwa mara ya kwanza kabisa.
Timu ya Wanawake ya Cameroon ilitajwa kua Timu bora ya soka ya wanawake huku Mwanamke bora miongoni mwa wachezaji waliotia fora akiwa Perpetual Nkwoche wa Nigeria.
-BBC