Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa 18 wa Hali ya Siasa Tanzania unaofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, Desemba 16, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wadau waliohudhuria Mkutano wa 18 wa Hali ya Siasa, kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET, ulioanza Desemba 16, katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP, Said Sud Said, Desemba 16 wakati akiagana na wadau waliohudhuria Mkutano wa 18 wa hali ya Siasa Tanzania, unaofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kuhusu Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET.
Baadhi ya wadau waliohudhuria Mkutano wa 18 wa Hali ya Siasa Tanzania, wakipiga picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa mkutano huo ulioanza Desemba 16, katika Ukumbi wa Ubungo Plaza na kujadili Demokrasi na Mageuzi ya Kijamii Tanzania, ulioandaliwa na Taasisi ya REDET. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR