Na Mwandishi Wetu
TIMU ya kombaini ya Coca Cola iliyotokana na michuano ya Copa Coca Cola inaondoka kesho alfajiri (Desemba 17 mwaka huu) kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kwenye kambi maalumu ya mafunzo ya mpira wa miguu.
Wachezaji 14 wanaoondoka ni Peter Manyika, Abdul Mgaya, Pascal Matagi, Mohamed Hussein, Mbwana Ilyasa, Farid Musa, Suleiman Bofu, Salvatory Raphael, Paul James, Miraji Adam, Kapeta Mohamed na Basil Seif.
Mafunzo hayo yataanza Desemba 18 mwaka huu, na timu itapata fursa ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki. Timu hiyo itarejea nchini Desemba 22 mwaka huu.
Desemba 21 mwaka huu timu hiyo ya Copa Coca Cola itashuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) kati ya Orlando Pirates na Golden Arrows itakayochezwa Johannesburg.
Viongozi watakaondamana na timu hiyo ni pamoja na kocha Kim Poulsen, daktari Joakim Mshanga na ofisa kutoka kampuni ya Coca Cola ambayo ndiyo imeandaa na kugharamia safari hiyo.