MIAMBA ya masumbwi nchini, Bingwa wa Mabara, Francis Cheka (SMG) na Bingwa wa Dunia, Karama Nyilawila (Captain) wanatarajia kupanda ulingoni Januari 28 mwaka huu, kupimana nguvu kati ya mabingwa hao.
Kihistoria mabingwa hao yaani Cheka pamoja na Nyilawila hawajawahi kutwangana jambo ambalo limekuwa likizua minong’ono kwamba huwenda mabondia hao wanaogopana.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam promota wa pambano hilo, Philemon Kyando ‘Don King’ alisema pambano hilo litafanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ambapo ni nyumbani kwa bondia Cheka. Alisema pambano hilo litakuwa na raundi 10 uzito wa kg 72.
Aidha akiyataja mapambano mengine ya awali amesema bondia Maneno Osward (mtambo wa gongo) atazichapa na Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.
Hata hivyo, Promota huyo amesema lengo la kumuandalia pambano bondia Nyilawila na Cheka ni kuondoa uvumi kuwa mabondia hao wanaogopana, lakini pia kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini.
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Mkoa wa Kimichezo wa Ilala, Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
Chanzo:Super ‘D’ Boxing Coach