TFF yawataja 37 watakao shiriki semina ya Grassroots

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura

Na Mwandishi Wetu

WASHIRIKI 37 wameteuliwa kushiriki katika semina ya grassroots inayolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam itakayofanyika kuanzia Desemba 14-17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo, leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema, mbali ya walimu wa shule za msingi ambao ndiyo wengi, washiriki wengine wanatoka Kamati za TFF za Mpira wa Miguu ya Vijana na Mpira wa Miguu wa Wanawake.

Wambura amesema semina hiyo itakayokuwa chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gouinden Thondoo kutoka Mauritius ambaye ameshawasili nchini itamalizika Desemba 17 mwaka huu kwa tamasha (festival) litakalofanyika Uwanja wa Taifa na kushirikisha watoto 1,200.

Aidha ameongeza kuwa washiriki wa semina hiyo ni Maria Tarimo, Magreth Mainde, Isaac Muhanza, Lucian Boniface, Hassan Msonzo, Hadija Kambi, Charles Kiwero, Abdul Mwarami, Florence Ambonisye, Sophia Willbest, Muhidin Manish, Rajab Asserd, Rebecca Joseph, Mussa Kapama, Rukia Mkai, Phoebe Lugana na Imani Mwalupetelo.

Wengine ni pamoja na Idd Luena, Dina Muhomba, Ally Chanda, David Kivinge, Juma Ally, Seif Koja, Raymond Gweba, Farij Bukuji, Gema Matagi, Joyce Sanka, Stella Seng’ongo, Hassan Seleman, Ramadhan Yahya, Maua Rashid, Paul Chagonja, Ali Mtumwa, Daud Yassin, Michael Bundala, Raphael Matola na Furaha Francis.