Na Mwandishi Wetu
MPANGO wa AfrikaKujitathmini Kiutawala Bora (APRM) unaotekelezwa hapa nchini, umetajwa kuwanyenzo muhimu ya kusaidia nchi kuimarisha utawala bora. Hayo yalielezwa jijiniDar es Salaam na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wananachi wa kawaidawalipotembelea maonesho ya miaka 50 ya uhuru.
Makamu wa Kwanza waRais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akitembeleaWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wizara inayounganishashughuli za APRM hapa nchini, alishauri kuwa ni muhimu zaidi maoni hayo yawananchi yakatekelezwa.
Akimweleza kiongozihuyo kuhusu mchakato wa APRM, Ofisa Habari na Mawasiliano wa APRM Tanzania, Bw.Hassan Abbas alisema maoni ya wananchi yaliyokusanywa kupitia utafiti wa APRMnchini yataanza kufanyiwa kazi mara baada a mwakani.
“Kwa mujibu wa mchakatohuu, nchi inapomaliza kujitathmini, kiongozi wan chi husika huiwasilisha ripotiya nchi yake mbele ya wakuu wenzake wan chi za Afrika kwa ajili ya kupeanaushauri mbalimbali,” alisema Bw. Abbas.
Naye Makamu wa Pili waRais katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi alisisitiza juuya umuhimu wa APRM kuwaelimisha zaidi wananchi hasa visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa ripotiiliyohuishwa hivi karibuni ya APRM Tanzania, Tanzania kwa ujumla imeonekanakupiga hatua kubwa katika kuboresha misingi ya kisera na kisheria katika kukuzautawala bora nchini, ushiriki wa umma katika masuala ya uongozi na utawalaumeimarika na nguvu za mihimili ya dola katika kuhakikisha nchi inakuwa imarazimeimarishwa.
Hata hivyo ripoti hiyoimeonesha kuwa wananchi na wataalamu mbalimbali waliohojiwa wameshaurikushughulikiwa changamoto mbalimbali zikiwemo kero za Muungano, tatizo la uchumimpana kutowafikia wananchi wengi na suala la katiba mpya.
APRM ni taasisiiliyobuniwa na viongozi wa nchi za Afrika (AU) mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwalengo la kuwashirikisha wananchi kuainisha mazuri ya utawala bora katika nchizao ili yaimarishwe zaidi na pia kutaja changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi.
Tanzania ni miongonimwa nchi 30 kati ya 54 za Afrika zilizoridhia mkataba wa kuanzishwa mpango waAPRM na hapa nchini taasisi hii iko chini ya Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa.
Ripoti za APRM kutoka kila nchi mwanachama mbali yakuwasilishwa mbele ya wakuu wa nchi zinazoshiriki mpango huo kwa ajili yakupeana uzoezi na kushauriana pia huandaliwa mpangokazi wa kitaifa wa miakamitatu mitatu kwa ajili ya Serikali husika kufanyiakazi changamotozilizobainishwa. Kwa mujibu wa mkataba, utafiti huu hurudiwa kila baada yamiaka minne.