Urusi kwachafuka, maelfu waandamana

Baadhi ya waandamanaji wafuasi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo zamani, Mikhail Kasyanov wakivutana na polisi katika moja ya maandamano ya nyuma nchini humo.

MAELFU ya wananchi nchini Urusi wameandamana katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo wakishinikiza kurudiwa kwa Uchaguzi wa Bunge uliofanywa Jumapili iliyopita nchini humo.

Taarifa kutoka ndani ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Moscow, zinasema maandamano makubwa yamefanywa katika Mji huo, ambako mwandishi wa BBC, anasema maelfu ya watu wako katika medani, ng’ambo ya pili ya mto, mkabala na Ofisi za serikali.

Akihutubia watu wanaopeperusha bendera, Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi, Mikhail Kasyanov, alisema watu wamechoka kuendeshwa kama ng’ombe.

Taarifa zaidi zinasema maandamano mengine madogo yamefanywa sehemu nyingine za Urusi, ikiwemo St. Petersburg, ambako kulizuka pia msukumano kati ya polisi na waandamanaji.

Waandamanaji wanadai kulikuwa na udanganyifu mkubwa katika uchaguzi wa Jumapili iliyopita, ambapo chama tawala cha United Russia kiliongoza.
-BBC