Golikipa wa Timu ya Taifa ya Rwanda, Ndori Jean Claude akijiandaa kuzuia mpira wa hatari uliyokuwa ukitaka kuzitikisa nyavu za goli lake.
Mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uganda, Sula Matovu akijiandaa kuingiza krosi langoni mwa wapinzani wao. Katika mchezo huo wa fainali Uganda ilishinda kwa mikwaju ya penati 5-4.
Mchezaji Kavuma Habib wa Timu ya Taifa akijaribu kuuwahi mpira wa hatari uliopigwa kuelekea katika lango lao katika mpambano wa Fainali kati ya timu yao na Rwanda.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uganda (wenye flana za njano na nyeusi) wakiwapa pole wenzao wa Rwanda baada ya mchezo kumalizika na Uganda kuibuka washindi kwa mabao 5-4, Uganda walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la CECAFA Tusker Chalenji 2011.
Uganda wakiwapa pole wenzao wa Rwanda baada ya mchezo kumalizika na Uganda kushinda
Timu ya Uganda ikishangilia baada ya kukabidhiwa Kombe la Tusker Chalenji, mfano wa hundi ya dola 30,000 za Marekani. Hapa wakipata picha ya viongozi pamoja na wadhamini wakuu wa kombe hilo Serengeti Breweries (SBL)
Mashabiki wa Timu ya Uganda wakipagawa kushangilia mara baada ya kunyakuwa kombe la Tusker. (Picha zote na Joachim Mushi wa dev.kisakuzi.com)