Naibu Waziri wa Fedha, Silima atembelea Banda la Benki ya Twiga Bankorp

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Pereira Silima akimsikiliza Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bankorp, Adarbert Mchunguzi Tibikunda (kushoto) akimpa maelezo mbalimbali kuhusiana na huduma za Benki hiyo pamoja na ushiriki wa Beki ya Twiga katika Maonesho ya miaka 50 ya Uhuru kwa Wizara na taasisi za serikali yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri huyo wa Fedha, Silima aliisifu Benki hiyo kuhimili ushindani pamoja na kuunga mkono wazo la kushirikiana na Shirika la Posta nchini katika kufikisha huduma zake katika maeneo mengi nchini. (Picha na Mpigapicha wetu).

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Pereira Silima akitoka katika banda la Twiga Bank baada ya kutembelea banda hilo jana na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanya na Benki hiyo inayomilikiwa kwa asilimia 100 na serikali na inajiendesha yenyewe bila ruzuku ya serikali kuu. Beki ya Twiga nimongoni mwa taasisi za serikali zinazoshiriki katika Maonesho ya miaka 50 ya Uhuru yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Mpigapicha wetu).