Mtuhumiwa wa uhujumu uchumi amkataa hakimu

 

Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy Prof. Rick Mahalu.

NA Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala na Fedha, Grace Martin, wamewasilisha ombi la kumkataa hakimu anayesikiliza kesi yao ya uhujumu uchumi ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 2.

Kesi hiyo iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana washitakiwa hao walitakiwa kuanza kujitetea, lakini kabla ya jambo hilo wakili wa Mahalu, Mabere Marando kwa niaba pia ya mshitakiwa wa pili aliiomba mahakama hiyo mbele ya hakimu ambaye sasa ni jaji Sivangilwa Mwangesi kuwasilisha ombi la wateja wao.

”Wateja wetu wametuagiza tuseme haya, kwamba ujiondoe kusikiliza kesi hii na wametupa sababu saba zilizowafanya kukuomba kujiondoa,” alidai marando mbele ya hakimu huyo.

Akizitaja sababu hizo, marando alidai kuwa sababu ya kwanza ni kwamba kuna wakati upande wa mashitaka waliiomba mahakama kuendesha kesi kwa njia ya mtandao yaani shahidi kutoa ushahidi kwa njia ya video akiwa nchini Ital, Roma na mahakama ikiwa Dar es Salaam, upande wa utetezi ulipinga lakini hakimu huyo alikubali ushahidi huo kutolewa.

Alidai kwa kufanya hivo, Serikali kupitia bunge ulifanya marekebisho kufanyika uhalali lilipitisha mushwada ambao kuruhusu ushahidi kwa njia ya video kuchukuliwa, mshitakiwa Mahalu akiwa ni mwanasheria aliona kuwa kuamuzi ule wa Mwangesi ulikuwa ni wa makusudi.

Sababu ya pili alidai kuwa hakimu huyo kwa kuruhusu shahidi kutoa ushahidi akiwa Ital ambapo ni nje ya mamlaka yake kitendo hicho kama mwanasheria ilikuwa ni kufanya makusudi.

Sababu nyingine alidai jamuhuri iliwasilisha mahakamani mkataba wa mauzo ambao ni kivuli, utetezi ulipinga nyaraka hiyo kupokelewa kama kielelezo kwa kuwa ni kivuli lakini mahakama ilipokea kwa madai kuwa aliyeitoa alisema kuwa kwa sheria ya Ital inaruhusu, wateja wao wanasema kuwa hakimu huyo asingeweza asingeweza kufanya maamuzi hayo ila ilikuwa makusudi.

Aidha wanadai washitakiwa walitaka kuonyeshwa maelezo ya mlalamikaji mwanzo wa kesi lakini upande wa mashitaka hawakuwa na mlalamikaji, hakimu huyo aliwalazimisha kuleta maelezo yake ambapo walileta maelezo na shahidi huyo ambaye hakuwepo katika mashahidi wao jambo hilo wamelitafsiri hakimu alilazimisha, na kwamba kesi ingefutwa kwasababu hakukuwa na mlalamikaji.

Sababu nyingine ni kwamba upande wa mashitaka ulipofunga ushahidi utetezi ulitaka kuwasilisha hoja zao za washitakiwa hawana kesi ya kujibu lakini hakimu huyo hakuzingatia rai hiyo badala yake alitoa uamuzi hapo hapo mezani kwamba washitakiwa wana kesi ya kujibu uamuzi ambao uliwafadhaisha sana.

Sababu ya mwisho walidai kuwa serikali ilitamka bungeni kuwa ubalozi wa Ital ulinunuliwa kwa mujibu wa sheria na wizara ya mambo ya nje haikuwa na malalamiko kauli iliyotolewa na waziri wa wizara hiyo, washitakiwa waliamini kwa kauli hiyo ingekuwa ni ushawishi mkubwa mahakamani kuwaona washitakiwa hawana kesi ya kujibu.

Marando alidai sababu ya saba wanaiacha na alimaliza kwa kudai kuwa washitakiwa wanadai kuwa wana woga kwamba wasipate haki kupitia hakimu huyo ambaye sasa ni jaji na kwamba ajitoe ili hakimu mwingine ateuliwe kusikiliza kesi hiyo.

Upande wa mashitaka ukijibu hoja hizo ulidai kuwa maombi hayo yamewashitua kwasababu mambo mengi ni ya nyuma sana na baadhi ya sababu washitakiwa walishazikatia rufaa na uamuzi kutolewa. Hakimu amepanga kutoa uamuzi huo Machi 28 mwaka huu.
Mwisho