Jaji Warioba atembelea Banda la Wizara ya Fedha

Ofisa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Simoni Masawe (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) juu ya jitihada mbalimbali zinazotumiwa na Mamlaka hiyo katika kuwaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi. Waziri Mkuu huyo alipata maelezo hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) akiangalia machapisho mbalimbali ya Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) yanayoonyesha fursa mbalimbali ambazo mwananchi anaweza kuzipata kupitia Benki hiyo katika kujikomboa kiuchumi. Waziri Mkuu huyo alipata maelezo hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. (Picha zote na Tiganya Vincent, MAELEZO-Dar es Salaam)

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu ya Tanzania (TIA) jana jijini Dar es salaam alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. (Picha zote na Tiganya Vincent, MAELEZO-Dar es Salaam)